Manchester United wameondoka kwenye mkia katika kundi
lao la ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, baada ya kupata ushindi dhidi ya
Zorya Luhansk.
Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la pekee dakika ya
69, baada ya kombora la nguvu mpya Wayne Rooney kugonga mlingoti wa goli.
Hilo ndilo bao la kwanza la Ibra katika mechi tano,
na lilitokana na kombora la kwanza la United lililolenga goli kwenye mechi
hiyo.
Mashetani hao Wekundu walitarajiwa kufanya vyema
Europa League lakini walianza kampeni yao kwa kulazwa 1-0 na klabu ya Feyenoord
ya Uholanzi mechi yao ya kwanza.
United sasa wamo katika nafasi ya tatu katika kundi lao wakiwa na
alama sawa na Feyenoord na moja nyuma ya viongozi Fenerbahce wa uturuki ambao
watazuru Old Trafford 20 Oktoba.
Post a Comment