Kuelekea katika mchezo wawatani wa jadi kati ya
klabu ya soka ya Simba dhidi ya Yanga mashabiki wa klabu ya soka ya Yanga
wamefunguka na kuelezea mwenendo wa klabu yao kabla ya mchezo wao huo.
Mashabiki hao wamesema kuwa
pamoja na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya klabu ya Stand United kwa
kutandikwa bao 1 kwa nunge wamesema kuwa kuelekea katika mchezo wao lazima
wataifunga klabu ya soka ya Simba.
Mchezo wa watani wa jadi huo unatarajiwa kupigwa
katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam jumamosii huku macho na
masiki ya wapenzi wa soka nchini na nje ya nchi yakielekea katika kipute hicho.
Post a Comment