Kamati ya mashindano ya chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA ipo
katika maandalizi ya mwisho ya ligi kuu ya soka visiwani humo kwa msimu wa
2016/17 ambao umepangwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Katibu mkuu wa ZFA Kassim Hadji Saloum amesema kwa sasa kamati
ya mashindano inakamilisha baadhi ya taratibu za mwisho ambazo zitatyoa taswara
tofauti ya mshike mshike wa ligi ya msimu huu ambao bado utashuhudia ligi
ikichezwa katika kanda ya Unguja na Pemba kabla ya kuingia kwenye hatua ya
fainali.
Hata hivyo KAssim Hadji Saloum ametoa wito kwa wadau wa soka wa
ndani nan je ya Zanzibar kujitokeza kwa ajili ya kudhamini ligi hiyo ambayo
wakati mwingine imekua ikikosa msisimko kutokana na ukata wa fedha.
Post a Comment