Kiungo wa klabu ya soka ya Arsenal Santi Cazorla amesema
anapenda kuendelea kubaki kunako katika klabu hiyo lakini anasubiri kuona kama
atapewa mkataba mpya.
Cazorla, mwenye miaka 31, yupo huru kuongea na klabu
nyingine yoyote mwezi January wakati mkataba wake unakaribia kuisha mwishoni
mwa msimu huu.
Lakini raia huyo wa nchini Hispania amebainisha nia
yake ya kutaka kuendele kubaki klabuni hapo na kupewa mkataba mwingine.
Cazorla alijiunga na Arsenal akitokea Malaga mwaka
2012 na amefunga mabao 29 mara zote katika mashindo 177 aliyocheza.
Post a Comment