Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Manchester United Jose
Mourinho amesema kuwa wachezaji wake wataonyesha maajabu hivi karibuni ya
kufanya vyema kwa mashabiki na kuifanya klabu yao kuwa moja ya klabu inayofanya
vyema zaidi.
Bisi huyo wa Old Trafford ameita kikosi cha
wachezaji 26 katika msimu huu lakini wachezaji wake wamekuwa katika wakati
mkgumu zaidi katika msimu huu.
Mchezaji wake Matteo Darmian hayupo katika hali nzuri,
Morgan Schneiderlin bado hajarea kucheza katika ligi hiyo huku mchezaji Memphis
akicheza dakika 88 pekee katika kikosi chao.
Lakini Mourinho amesema anahitaji muda zaidi kuona
wachezaji wake wakicheza na kuwafahamu zaidi wachezaji wake na anaimani ataleta
maajabu hivi karibuni.
Post a Comment