TIMU ya Soka ya Taifa ya TANZANIA umri chini ya
miaka 17 Serengeti Boys kesho inashuka dimbani kukipiga dhidi ya timu ya vijana
ya Congo Brazzaville ukiwa ni mchezo muhimu wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa Vijana 2017 nchini Madagasca.
Serengeti Boys inayonolewa na kocha Bakari Shime
inacheza mechi hiyo baada ya awali kushinda mabao 3-2 nyumbani kwenye Uwanja wa
Taifa, na ikiitoa Congo itakuwa imefuzu kucheza fainali hizo za Afrika.
Serengeti ikifanya vizuri itafuzu kushiriki fainali
hizo za 12 za michuano hiyo ya vijana baada ya kuwa kambini ya siku 10 nchini
Rwanda kujiandaa na mchezo huo..
Post a Comment