Klabu ya soka ya Barcelona imetangaza kuwa itamkosa
beki wake Jordi Alba katika mchezo wa El Clasico aliyepata majeraha ya goti na
kifundo cha mguu katika mechi ya La Liga dhidi ya Real Sociedad.
Alba alipata majeraha hayo katika kipindi cha kwanza
cha mechi waliyotoa sare ya 1-1 katika dimba la Anoeta na hali hiyo imemwacha
beki huyo wa kushoto akihaha kupona kwa ajili ya El Clasico dhidi ya Real
Madrid wikiendi hii.
Vipimo vilivyofanyika asubuhi hii vinadhihirisha kuwa
Jordi Alba amepata majeraha kwenye goti lake la kulia na kwenye kifundo cha
mguu wa kushoto.
Hata hivyo, kiungo Arda Turan imethibitika yupo fiti
baada ya kukosa mechi ya wikiendi.
Post a Comment