Pambano la masumbwi lisilo na ubingwa kati ya bondia
Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ na Francis Cheka lililopangwa kufanyika Desemba
25, mwaka huu litakuwepo kama lilivyopangwa.
Pambano hilo ambalo litapigwa kwenye ukumbi wa PTA
Sabasaba jijini Dar es salaam, lilikuwa kwenye sintofahamu baada ya kukumbwa na
mgogoro kwa upande wa waandaaji.
Promota wa mapambano hayo Kaike Silaju amesema kuwa
maandalizi yote kuelekea katika pambano hilo yamekamilika na wapenzi wa mchezo
huo wasubiri burudani tuu kutokana na mabondia wote kujiaandaa vyema.
Naye mmoja wa mabondi wa pambano hilo Twaha Kiduku
amesema kwa upande wake amejipanga vyema sana kuelekea katika pambano hilo na
anaimani anaweza kumshinda mpinzania wake.
Post a Comment