Klabu ya soka ya Toto Afrika ya jijini Mwanza
inakaribia kumalizana mazungumzo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand
United Muhibu Kanu kuchukua nafasi ya Ukocha ndani ya klabu hiyo.
Kanu amesema kuwa kwa sasa anawasubiria Toto Afrika
kujua wanamipango gani kutokana na kufikia muafaka wa asilimia kubwa kuweza
kutua klabuni hapo kuifundisha timu hiyo au kuchukua kitengo cha ukurugenzi wa
ufundi wa klabu hiyo.
Amesema mbali na klabu hiyo lakini ametoa mualiko wa
klabu zingine za Ligi kuu zinazomuhitaji waweze kupeleka ofa zao.
Post a Comment