Riphat ambaye ni mshambulaji
aliwashinda wachezaji Shaban Idd wa Azam FC na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.
Katika mechi mbili ambazo timu ya
Ndanda FC ilicheza kwa mwezi huo, Riphat aliisaidia timu yake kupata ushindi
katika michezo yote na kukusanya jumla ya pointi 6 zilizoifanya kushika nafasi
ya kumi katika msimamo wa Ligi hiyo ambayo iko mapumzikoni kupisha dirisha dogo
la usajili.
Pia aliifungia timu yake mabao
mawili katika michezo miwili ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo.
Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili
zilizochezwa. Kwa kushinda tuzo hiyo, Riphat atazawadiwa kitita cha sh. milioni
moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
Post a Comment