Na Najaha Bakari.
Baraza la michezo Taifa BMT limetoa wito kwa wanachama
wa chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania CHAKUTA kujitokeza kwa wingi kuchukua
fomu za kuwania nafasi mbalimbali za
Uongozi ndani ya chama hicho.
Uchaguzi wa chama cha mchezo wa kuogelea unatarajia
kufanyika Oktoba 10 mwaka huu mjini Morogoro na mwisho wa kurudisha fomu ni
Oktoba 30 mwaka huu.
Katika uchaguzi huo nafasi zinzowaniwa ni nafasi ya
Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,katibu Mkuu,katibu Msaidizi Mweka Hazina na Mweka
Hazina Msaidizi huku gharama za kuchukua fomu za nafasi hizo zikiwa ni
sh.200,000.
Huku nafasi zingine zikiwa ni za wajumbe wa kamati yay
a utendani wa chama hicho na kiasi cha kuchukulia fomu katika uchaguzi huo ni
sh.100,000.
Post a Comment