
Siku chache baada ya kupewa mkataba wa
kendelea kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kocha CHARLES
BONIFACE MKWASA kamati ya ufundi ya Shirikisho la soka nchiniTFF inatarajiwa
kufanya kikao cha kutafuta kocha mpya wa kukinoa kikosi cha Timu ya Taifa ya
vijana umri chini ya miaka 15.
Afisa maendeleo wa mpira wa vijana kutoka TFF JEMEDARI SAID amesema
kamati ya ufundi bado haijaketi kujadili ni kocha gani ambae atakuwa wa kudumu
kukifundisha kikosi hicho.
Timu ya Taifa ya vijana
tayari imevunja kambi yake ya kila mwezi iliyoweka katika hostel za karume na
kurudi masomoni kuendelea na masoma baada ya kutoka katika ziara walizoenda
kucheza na timu mbalimbali za mikoa ya Tanga na Arusha.
Post a Comment