
Kocha msaidizi wa Manchester United, mkongwe Ryan Giggs ameamua kumpa onyo
kinda MEMPHIS
DEPAY kutokana na mwenendo wake ndani ya Manchester United hivi sasa.
Manchester United walitoa
pauni milioni 25 kwa kijana huyo kutoka
PSV Eindhoven lakini alitolewa nje muda wa mapumziko Manchester United
ikiadhibiwa na Arsenal kwa magoli 3-0 wiki iliyopita.
Chanzo kimesema kuwa Depay
baada ya mchezo wa Arsenal alionekana usiku akila bata huku akionesha kutojali
kwa mambo yanayoendelea uwanjani.
Giggs ametoa onyo kwa kijana
huyo kutuliza akili na kufikiria zaidi uwanjani kuliko nje ya uwanja.
Giggs amesema hayo huku
akimkumbuka kocha wake Sir Alex Ferguson aliyekua mkali sana kwa wachezaji aina ya Depay.
Post a Comment