Mwenyekiti wa TASWA JUMA PINTO amesema tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka kwa mwaka huu zitakuwa tofauti kidogo kwani zitatumika kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kumpa tuzo ya heshima kwa kuthamini mchango wake katika kipindi cha miaka 10 aliyokuwa madarakani.
Awali tuzo hizo zilikuwa
zifanyike Oktoba 8 ila kwa sasa zitafanyika Oktoba 12, pamoja na tuzo hiyo ya
heshima lakini kuna tuzo 10 za wachezaji bora waliofanya vizuri katika kipindi
cha miaka 10, tuzo 5 kwa viongozi wa michezo na taasisi iliyochangia kukuza
michezo katika kipindi cha miaka 10.
Post a Comment