Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

SCHWEINSTEIGER KUONGEZA MAJERUHI MAN UNITED.



 
Kiungo mjerumani Bastian Schweinsteiger ameongeza idadi ya majeruhi kwenye klabu ya Manchester United hivi sasa baada ya kuumia jana mazoezini akiwa na timu yake ya taifa.

Nahodha huyo wa ujerumani alishindwa kuiwakilisha timu yake ya taifa katika mchezo wa makundi wa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya ulaya EURO 2016 baada ya kuumia ankle dakika chache akijiandaa na mazoezi.

Bastian anaungana na nahodha wa Manchester United na England, Wayne Rooney ambaye naye atakosa michezo miwili itakayochezwa na England leo Ijumaa na wiki ijayo kwa kuwa majeruhi.

United pia iko katika hali mbaya baada ya mlinzi wake muargentina Marcos Rojo naye kutokua fit kucheza na hatimaye akaenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina.

Bado haijafahamika kama wachezaji hao watakua fit tayari kuiwakilisha United katika mchezo mgumu dhidi ya Everton Oktoba 17.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget