PACQUIAO YUKARIBU KUSTAAFU MASUMBWI.
Pacquiao,ambaye alipoteza kwa Floyd Mayweather katika pigano la mwisho ,anataka kuwania kiti kimoja katika bunge la seneti mwaka 2016.
Pacquiao amesema kuwa hawezi kusema iwapo pigano lake la mwisho litakuwa dhidi ya Mayweather,baada ya raia huyo wa Marekani kuahidi kustaafu baada ya ushindi wake dhidi ya Andre Berto.
Raia huyo wa Ufilipino ,ambaye alifanyiwa upasuaji katika bega lake baada ya pigano lake na Mayweather,anajivunia rekodi ya mapigano 57,kushindwa mara 6 na sare ya mapigano 2.
Post a Comment