
Nahodha wa kimataifa wa
England WAYNE ROONEY atakosa mchezo wa kuwania tiketi ya fainali za Euro 2016
dhidi ya Estonia
baada ya kupata jeraha wakati alipoichezea Manchester United.
Mshambuliaji huyo hakufanya
mazoezi na kikosi cha ROY HODGSON tangu walipokutana Jumanne lakini licha ya
kukosa mchezo huo ataendelea kuwa na timu hiyo hadi utakapowadia mchezo
mwingine dhidi ya Lithuania.
Beki wa Chelsea GARY CAHILL
ndiye atakayetwaa mikoba ya unahodha baada ya ROONEY kuondolewa katika nafasi hiyo
kwa muda.
Post a Comment