
Baada ya kuanza vizuri kwa
timu ya Taifa Tanzania Taifa
Stars kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Malawi
(The Flames) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaaam siku ya jana kikosi
hicho kinatarajia kuondoka kesho nchini kuelekea Lilongwe
Malawi.
Stars inaelekea nchini Malawi
kucheza na timu hiyo ukiwa ni mchezo wao wa marudiano wa kusaka tiketi ya
kufuzu fainali za Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Uswiz mchezo
utakopigwa Oktoba 9 mwaka huu.
Afisa habari wa TFF BARAKA KIZUGUTO amesema timu hiyo inaelekea
nchini Malawi
siku ya kesho ikiwa na wachezaji wake 24 pamoja na benchi la ufundi likiongozwa
na kocha Mkuu CHARLES BONIFACE MKWASA.
Naye Rais wa TFF JAMALI
MALINZI amekipongeza kikosi cha Stars kwa ushindi huo na kuwataka watanzania
kuendelea kuwasapoti katika mchezo wao huo wa marudianio nchini Malawi.
Post a Comment