Kocha
Mkuu wa klabu ya soka ya JKT Ruvu Abdallah
Kibadeni amekiri na kuwa safu yake ya ushambuliaji kikosini hao kuwa nib utu na
inatakiwa ifanyiwa marekebisho ya haraka zaidi.
Kibadeni
ameyasema hayo baada ya kutoka nayo sare ya bila kufungana na klabu ya soka ya
Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa katika
dimba la uwanja wa karume jijini Dar es Salaam juzi.
Amesema
kikosi cha hivi sasa kinawachezaji wengi wapatao 30 na kinaitaji marekebisho
makubwa ya kufumua kikosi cha kwanza ili kupata kikosi ambacho kitakuwa imara
zaidi katika ushindani wa ligi kuu.
Kibadeni
amechukua nafasi ya Fred Minziro aliyejiuzulu kutokana na matokeo mabovu ya
timu hiyo.
Lakini
paoja na matokeo hayo klabu ya JKT Ruvu ipo mkiani mwa ligi kuu ikiwa na pointi
mbili tu katika mechi saba ilizocheza hadi sasa.
Post a Comment