Ligi Kuu soka Tanzania Bara inatarajiwa
kuendelea tena siku ya kesho kesho kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja
mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa huku kila timu ikisaka ushindi
wa pointi tatu muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Simba SC watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga, mchezo utakaonza
majira ya saa 10:30 jioni.
Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United
uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Wachimba Almasi wa Mwadui FC
watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Toto African watakua wenyeji wa maafande
wa Mgambo Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar
watakua wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex mkoani
Morogoro.
huku watoza ushuru wa jiji la Mbeya
katika uwanja wa Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa Majimaji kutoka mkoani
Ruvuma.
Post a Comment