Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles
Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 28 wa timu ya taifa kilicho
tayari kupambana na Algeria.
Stars itaivaa Algeria katika mechi mbili mfululizo
kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018, ikianza kwa kupambana nayo Novemba 17
jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17, ugenini.
Mkwasa amewaongeza kikosini washambuliaji Malimi
Busungu wa Yanga SC na Elias Maguri katika kikosi kitakachomenyana na Algeria
katikati ya mwezi ujao.
Mkwasa ametaja wachezaji 28 ambao wataoingia kambini kwa
siku 10 nchini Oman kuanzia Novemba 1, mwaka huu kujiandaa na Algeria katika
hotel ya Urban Rose.
Taifa Stars itamenyana na Algeria katika hatua ya
mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe
la Dunia 2018 Urusi, baada ya kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza.
Wachezaji hao kuwa ni makipa; Aishi
Manula (Azam FC), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa
Sugar).
Mabeki ni: Shomary Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan (Yanga SC), Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba SC) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar).
Viungo ni; Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba SC) na Salum Telela (Yanga SC).
Washambuliaji ni Mbwana: Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Free State Stars, A. Kusini), Farid Mussa, John Bocco (Azam FC), Simon Msuva, Malimi Busungu (Yanga SC), Elias Maguri (Ruvu Shooting) na Ibrahim Hajib (Simba SC).
Post a Comment