City wameshinda michezo sita kati ya debi nane za majuzi zaidi za Manchester United kuanzia ushindi wao wa 6-1 mwaka 2011.
Van Gaal anahisi kwa kuwa City ndio wanaoongoza Ligi ya Premia kwa sasa ina maana kwamba ndio wanaofaa kupigiwa upatu kushinda.
“Wanaongoza. Sisi tuko nambari tatu. Kuna tofauti kubwa ya mabao.Na tofauti ya alama na Wanapigiwa upatu wa kutwaa taji la ligi.”
Maneno hayo ya Van Gaal yanakaribiana sana na ya mtangulizi wake David Moyes kabla ya mechi ya Old Trafford dhidi ya mahasimu wengine wakuu wa United, Liverpool.
Meneja huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich anafahamu vyema sana umuhimu wa mechi hiyo ya wikendi hii kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Lakini licha ya uhasama wa kinyumbani kati ya City na United, Van Gaal amesisitiza kwamba hataingiza hisia kwenye mechi hiyo ndipo timu yake iwe na nafasi nzuri ya kushinda debi ya pili mfululizo Old Trafford.
Post a Comment