
Baada ya Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola kuamua kubwaga manyanga ya kuachana na kazi yake ya kuinoa klabu ya soka ya simba uongozi wa klabu hiyo umesema utaketi muda wowote kujadili hatima ya taarifa za kocha huyo.
Akizungumzia sakataa hilo Afisa
habari wa klabu ya soka ya simba HAJI MANARA amesema ni kweli kunataarifa za
kocha huyo kubwaga manya lakini wao kama klabu wataketi kujadili taarifa ambayo
kocha huyo ameiwasilisha kwa Rais wa klabu hiyo EVANS AVEVA.
Matola ambaye ni nahodha wa zamani
wa klabu ya soka ya Simba, alifanya kikao cha na Rais wa klabu hiyo Evans Aveva
lakini akashikilia msimamo wake wa kutaka kuachia ngazi.
MANARA amesema kilichopelekea Matola
kuachia nagzai ni kutoelewana na Kocha mkuu wa klabu hiyo Dylan Kerr katika
masuala mengi, jambo ambalo Matola halikumpendeza.
Kwa upande
mwingine MANARA ameelezea kuogeza mchezaji mwingine katika kikosi chao huku
ameitakia kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mchezo wao
wa jumamosi na kuwataka watanzia kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo.
Post a Comment