Kamati ya
uchaguzi ya Shirikisho la soka duniani FIFA limemuondoa katika kinyang’anyiro
cha Urais wa FIFA Musa Bility ambaye ni Rais wa chama cha soka cha nchini
Liberia.
Bility
amekuwa mmoja kati ya watu ambao wameomba kugombea nafasi ya Urais wa FIFA
kuchukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter ambaye
ameamua kujiuzulu hivi karibuni.
Kamati ya
uchaguzi imeamua kumuondoa Musa Bility kwa sababu za Uadilifu baada ya
kumchunguza na kujiridhisha kuwa Bility hana sifa ya kubaki kuwa mgombea wa
Urais katika uchaguzi mkuu wa FIFA mwezi wa pili tarehe 26 mwaka huu.
Mwingine
aliyeondolewa katika kinyang’anyiro hicho ni Rais wa UEFA Michel Platini.
Michel
Platini ameondolewa katika kuwania nafasi ya Urais kwa sababu amefungiwa na
kamati ya maadili ya FIFA kwa muda wa siku 90 kwa kosa la kuhusika kupokea
rushwa toka kwa aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter.
Post a Comment