Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars
CHARLSE BONIFACE MKWASA amewaondoa hofu watanzania katika mchezo wao wa kesho
dhidi ya Algeria utaopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mchezo wao huo wa kesho MKWASA amesema wachezaji
wake wote wapo na morali ya hali ya juu katika mchezo huo na atatumia mfumu
ambao ni rahisi kwa wachezaji wake kuutumia katika mchezo huo ili kuleta
matokeo mazuri zaidi.
Mkwasa amesema mpaka hii leo hana mchezaji yeyote
ambae ni majeruhi na amewataka watanzia kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo
ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.
Lakini kuelekea katika mchezo huo mashabiki
mbalimbali wa soka nchini wametoa maoni yao kuhusu mchezo huo huku wakiitaka timu yao ya
Taifa Stars kutoiogopa Algeria katika mchezo huo.
Post a Comment