
Tiketi za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za
Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria
ziataanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.
Magari maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi
hizo za mchezo kesho saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi
zinauzwa kwa shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na
rangi ya machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.
Vituo vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za
TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House –
Posta, Big Bone – Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala,
Uwanja wa Uhuru.
TFF imewaomba wadau, washabiki na watanzania
kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu
yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa
tiketi zisizokuwa halali.
Post a Comment