
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’
iliyorejea jana jioni ikitokea
chini Afrika Kusini ilipokuwa imeweka kambi ya siku kum leo jioni
itafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha
mzalendo Charles Boniface Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo
eneo la Posta jijini Dar
es salaam.
Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR wameungana kambini na wachezaji
wenzao jana na kufanya kikosi cha Stars kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.
Wapinzani wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria
wanatarajiwa kuwasili leo nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na watafikia katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni Ijumaa
watafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Wakati huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini
Mali, mwamuzi wa kati Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na
mwamuzi wa akiba Coulibaly Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi,
huku mtathimini wa waamuzi Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger
alishawasili nchini tangu juzi usiku.
Kamisaa wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini
Zimbambwe amewasili nchini leo mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini
(South Africa Airways)
Post a Comment