
Wachezaji wa kitanzania Thomas
Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaokipiga katika klabu ya Tp Mazembe ya nchini
Congo kesho wanakutana na kibarua kingine kugumu cha kuitetea klabu yao katika
fainali za kushiriki klabu bingwa Afrika.
Mchezo wa klabu ya soka ya TP
Mazembe utakuwa ni wa marudiano watakaocheza dhidi ya USM Alger ya nchini
Algeria.
Katika mchezo wa kwanza katika Uwanja
wa Omar Hamadi nchini Algeria klabu ya TP Mazembe ilishinda mabao 2-1, hivyo
huku kati ya hao moja likiwekwa nyavuni na Mbwana Samtta.
Lakini baada ya mchezo huo wa kesho Samatta
na Ulimwengu watajiunga na kambi ya Taifa Stars huko Afrika Kusini kujiandaa na
mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Algeria.
Post a Comment