
Baada ya klabu ya Simba,Yanga na Azam Fc kuwapa
mapumziko wachezaji wao nayo kalbu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro
umewapa mapumziko wachezaji wake kwaajili ya kupumzisha miili yao.
Akizingumza na Kilowoko.blogspot.com afisa habari wa
klabu hiyo Thobias Kifaru amesema wameamua kuwapa mapumziko wachezaji wao ili
kuwapa nafasi ya kujirekebisha mahali walipokosea katika ligi kuu soka Tanzania
bara.
Kifaru amesema mpaka hivi sasa bado wanaendelea kuwa
na upinzani wa kutosha katika ligi hiyo na kuwa klabu tishio pindi inapokuwa
uwanjani.
Mtibwa Sugar hivi sasa katika Msimamo wa ligi kuu soka
Tanzania bara inashika nafasi ya 3 huku ikikusanya point zake 22 katika ligi
hiyo.
Post a Comment