
Baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 siku ya jana
dhidi ya Mtibwa Suger sasa Kikosi cha
Azam Fc kinajiandaa kwenda Visiwani
Zanzibar kwaajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi huku kikipanga kuondoka na wachezaji 26 ambao
watashiriki michuano hiyo.
Afisa habari wa klabu hiyo Jafary Idd amesema baada
ya mchezo wao wa jana ambao ulikuwa wa vuta nikuvute sasa kikosi chake kipo
vizuri kwajili ya kupambana tena katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo
linahusisha na timu za kutoka nje ya Tanzania.
Kikosi cha Azam kinaelekea visiwani Zanzibar January
mosi kwajili ya michuano hiyo ambayo inasubiriwa na wapenzi wengi wa soka
visani humo kutokana na timu ambazo zinashiriki michuano hiyo.
Post a Comment