
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania
TFF Jamali Malinzi imebariki kamati ya nidhamu ya Shirikisho hilo baada ya kumchukulia
hatua Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha klabu ya soka ya Yanga Jerry Muro
baada ya kumtolea maneno ya kibaguzi Msemaji wa klabu ya soka ya Simba Haji
Manara.
Malinzi amesema kuwa msemaji wa klabu isiwe sababu
ya kufanya vitendo visivyo faa katika masuala ya mpira na kuingiza masuala
binafsi michezoni.
Malinzi amemuagiza Mkurugenzi Mkuu Wa Bodi ya Ligi
nchini Boniface Wambura kuwapa semina wasemaji wote wa vilabu vinavyoshiriki
Ligi kuu soka nchini Tanzania ili kupata uelewa wa jinsi ya kufanya kazi zao.
Post a Comment