Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

TFF YAOMBWA KUPEWA RUNGU NA WIZARA YA MICHEZO.



 

Shirikisho la Mpira nchini Tanzania TFF imeiiomba Serikali kwa kupitia Wizara ya habari,wasanii,utamauni na Michezo kushirikiana kwa karibu katika kuandaa timu za Taifa na kuboresha miundo mbinu ya michezo nchini ili kupata wachezaji wengi wenye vipaji wanotokea nchini kuanzia ngazi ya chini.


Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema kama wakipewa fursa na Serikali kuratibu na kusimamia mpira wa miguu katika mashindano ya Taifa ya shule za msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISETA) wanaamini wataongeza uweledi katika usimamizi huo na kuhakikisha vipaji vinaibuliwa kila mwaka kuliko ilivyo hivi sasa.

Katika hatua nyingine Malinzi ameelezea mipango na mikakati yao ya mwaka ujao katika kuboresha mchezo wa soka na kuufanya uwe mchezo ambao unaleta maendeleo kuanzia ngazi ya chini ya vijana ambako kuna vipaji vingi.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget