Mechi za Mzunguko wa 3 wa Kombe la FA, ambalo kwa sasa
linaitwa Emirates FA Cup ambalo huzikutanisha Klabu za Ligi Kuu England na
Daraja la kwanza Mechi zake zitachezwa mwishoni mwa wiki hii.
Mabingwa Watetezi wa michuano hiyo klabuu ya Arsenal
baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Jumamosi watakuwa katika
uwanja wao wa nyumbani wa Emirates kuwakaribisha Sunderland.
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu soka nchini England,
Chelsea, Jumapili watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na timu ya Daraja la
chini Scunthorpe United.
Jumamosi mashetani wekundu klabu ya Manchester
United watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Old Trafford kucheza na Sheffield
United, na Man City watakuwa ugenini kucheza na Norwich City.
Liverpool wao watafungua dimba Ijumaa wakiwa Ugenini
kuivaa Exeter City huku Jumapili Tottenham wakiwavaa Leicester City ambao wako
nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya England.
Post a Comment