
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa
Stars na klabu ya soka ya TP Mazembe ya DRC Congo Mbwana Samatta kesho
anasafiri kuelekea nchini Nigeria kushiriki katika sherehe za ugawaji tuzo za
mwana soka bora wa Afrika zilizoandaliwa na chama cha soka barani Afrika CAF.
Samatta anasafiri kesho alfajiri kuelekea Nigeria akiongozana
na katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Mwesigwe Selestini katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji
tuzo hizo zitafayika Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya sherehe hizo
Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Post a Comment