
Klabu ya soka ya Yanga na Azam leo
zitashuka kwenye dimba la Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kucheza mechi ya
michuano ya Kombe la Mapinduzi, Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvite
kutokana na ushindani wa timu zenyewe.
Kila timu inataka kuonesha ubabe kwa
mwenzie baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu bara mwaka jana
Klabu ya Azam inaongoza katika
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35 huku klabu ya Yanga ikishika nafasi ya pili
kwa kufikisha pointi 32.
Mechi ya leo pia inasubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka hasa kutokana na matokeo yaliyopita ya mechi hizo
ambapo Yanga iliifunga Mafunzo mabao 3-0 huku Azam ilipata matokeo ya sare ya
bao 1-1 dhidi ya Mtibwa.
Mechi nyingine itakayopigwa siku ya leo itakuwa kati ya Mtibwa na Mafunzo.
Post a Comment