Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

BAADA YA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI KUPITIA SASA STAND KATIKA HILI SIJUI MSIMU UJAO.




Mchezaji Peter Mutabuzi aliyeichezea Stand United dhidi ya klabu yake, Mutabuzi aliwakilishwa na kiongozi wa klabu yake ya sasa Frank Mchaki wa KMC.


Mchezaji huyu alikuwa anaidai klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 3,400,000/= lakini kikao kilikubaliana alipwe kiasi cha Tsh 2,000,000/= ndani ya mechi nane za ligi toka tarehe ya kikao 15.01.2015.

Ben Kalama ambaye alikuwa kocha wa makipa wa Stand United alikuwa anadai malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Tsh usd 1,350 aliwakilishwa na Fadhili Hussein yeye walikubaliana kuwa anarudishwa kwenye timu na watalipana huko huko madai yake.

Kuhusu madai yake kiasi cha dola 1,350 kamati iliamua kwa kuwa ni madai halali na mwakilishi amekiri hilo basi wakatwe kwenye vyao vya mapato na TFF.

Mathias Lule ya madai ya mishahara, posho na medical insurance kiasi cha Tsh 48,300,000/= aliwakilishwa na Fadhil Hussein. Ilikubaliwa ya kwamba alipwe kiasi cha usd 4,300.00 ambacho kimethibitishwa na kukubaliwa tayari na juu ya madai mengine watakaa na muajiri wake wa zamani na kuyajadili kuona namna ya kulimaliza suala hili. Fedha hiyo itakatwa kwenye vyanzo vyao vya mapato.

JAKI FOOTBALL ACADEMY dhidi ya Stand United kiasi cha shilingi 7,600,000. Jaki waliwakilishwa na Fadhil Hussein ambaye alisema deni wanaloidai Stand United ni kiasi cha Tsh 4,200,000/= na deni hili limekubaliwa na litalipwa na Stand United kwenye vyanzo vyao vya mapato toka TFF.

Mkurugenzi wa Ufuni wa Stand United Muhibu Kanu anayeidai mishahara, na posho klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 16,600,000/=. Makubaliano yamefikiwa kweli Muhibu anaidai Stand kiasi hicho na ameshaanza kulipwa kupitia Bodi ya ligi kiasi cha Tsh 2,600,000/= hivyo kiasi kilichobakia cha Tsh 14,000,000/= anaenda kujadiliana na muajiri wake kwa kuwa amerudishwa kazini.

Kesi kati ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Stand United Emmanuel R. Massawe dhidi ya Stand United anayeidai Klabu ya Stand United kiasi cha Sh 12,100,000/= imehairishwa kwa kuwa muhusika hakuwepo wala hakutuma muwakilishi.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget