
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana mwishoni mwa wiki na kupitia kesi, mashauri mbalimbali kuhusiana na usajili na mikataba ya wachezaji na viongozi mbalimbali chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Mandi.
Mchezaji Ndikumana Hamad wa Stand United, mwenyewe alikuwepo na pia aliwakilishwa na Fadhil Hussein.
Ndikiumana anaidai klabu ya Stand malimbikizo ya mshahara, malazi na chakula kiasi cha shilingi 11,025,000/=.
Na kamati hiyo pamoja na uongozi wa mchezaji huyo Wamekubaliana mchezaji anarudishwa kwenye klabu yake ya Stand United kuitumikia na pia madai yake watamalizana huko Stand na pia Stand imlipie gharama alizokuwa anaishi akiwa Dar es Salaam hotelini maana mchezaji sio raia wa Tanzania.
Post a Comment