
Uongozi wa Klabu ya Stand United ya
Shinyanga umeibuka na kudai kuwa hauna taarifa yoyote juu ya kuondoka kwa
wachezaji wao Haruna Chanongo na Abuu Ubwa kwenda kufanya majaribio kwenye timu
ya TP Mazembe ya Congo DR.
Hivi karibuni wachezaji hao
walitimkia katika klabu hiyo ya Congo DR kwa ajili ya kufanya majaribio ya siku
10, zoezi ambalo walilifanya na hatimaye kufanikiwa kufuzu huku hivi sasa
wakiwa wanasubiri kauli ya mwisho kutoka kwa mmiliki Moise Katumbi.
Afisa habari wa Stand United Deo
Makomba amesema amekuwa akisikia tu kwenye vyombo vya habari juu ya wachezaji
hao lakini haina taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kuondoka kwa wachezaji ho
kwanda kufanya majaribio TP Mazembe.
Akizungumza na Kilowoko.blogspot.com Makomba amesema kocha mkuu wa timu hiyo
Patrick Liewig amemwambia kwamba katika meza yake hakuna taarifa yoyote juu ya
kutokuwepo kwa wachezaji hao hao.
“Kocha Liewig amenidokeza kwamba
anashangazwa na kitendo cha wachezaji hao(Chanongo na Ubwa) kutojitokeza
mazoezini kwa kipindi kirefu, tena bila taarifa yoyote,”alisema Makomba.
Uongozi wa Stand unaonekana kuleta
sintofahamu kwa sababu hivi karibuni wakala wa wachezaji hao Fadhili Mtemi au
Mtaifa alizungumza na Kilowoko.blogspot.com
kwa njia ya simu na kukiri kwamba kila kitu kilikwenda sawa na kwamba
waliwasiliana na uongozi wa Stand kalbla ya wachezaji hao hawajaenda kuitumikia
klabu hiyo kuwa wakipata timu nje lazima klabu hiyo iwaruhusu.
Post a Comment