Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony amedai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya tetesi za yeye kutaka kuondoka Manchester City.
Hata hivyo alipohojiwa Bony amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa anafurahia kuwepo City kwani ni moja ya klabu kubwa nchini Uingereza.
Bony alijiunga na City kwa kitita cha paundi milioni 28 na kupewa mkataba wa miaka minne na nusu Januari mwaka jana.
Nyota huyo amefunga mabao nane katika mechi 23 alizocheza msimu huu lakini amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba toka mshambuliaji kiongozi Sergio Aguero aliporejea kutoka katika majeruhi Desemba.
Post a Comment