
Polisi mmoja wa Dubai anakabiliwa na kifungo cha
miezi sita jela na faini ya euro 124,000 kwa kutuma picha za video za pasi ya
kusafiria ya mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, katika mitandao ya
kijamii.
Polisi huyo wa Uwanja wa Ndege aliyejulikana kwa
jina la J.J anatuhumiwa na waendesha mashitaka kwa kuingilia mfumo wa
mawasiliano na alikiri kosa la kuvunja Sheria ya Mtandao lakini aliomba kusamehewa.
Messi alitua Dubai mwishoni mwa Desemba kuhudhuria
sherehe za tuzo ya Globe Soccer ambao alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
na polisi huyo aliomba kama anaweza kupiga picha na nyota huyo lakini
ilishindikana kwasababu alikuwa amechoka.
Polisi huyo mwenye umri wa miaka 26, baadae aliingia
katika chumba cha mawasiliano na kuirekodi video wakati Messi akionyesha pasi
yake ya kusafiria kwa wana usalama kabla ya kuituma katika mtandao wa Snapchat.
Post a Comment