
Baada ya kubwaga manyanga kwa aliyekuwa kocha msaidizi
wa klabu ya Ndanda FC Ngawina Ngawina ya Mkoani Mtwara uongozi wa klabu hiyo
sasa unajipanga kupata mbadala wake.
Katibu Mkuu wa Ndanda FC Suleimani Kachele amesema
alipata taarifa hizi kutoka kwa kocha mwenyewe baada ya kupigia simu na kudai
kuwa hatojihusisha na klabu hiyo kama kocha msaidizi.
Kachele amesema baada ya kocha huyo kubwaga manyanga
sasa kamati tendaji ya klabu hiyo itaketi muda wowote kuona jinsi gani
wanavyoweza kuweka mambo sawa katika klabu hiyo.
Kwa upande wake aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu
hiyo Ngawina Ngawina amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuambiwa yeye
anassbabisha klabu hiyo ipate matoikeo mabovu.
Ngawia amesema Ndanda ilipata matoke mabovu ilipofungwa
na klabu ya simba wiki iliyopita na klabu ya Azam hivyo kuambiwa yeye ndiye
aliyeuza timu.
Post a Comment