
Mabingwa watetezi wa kombe la Mfalme Barcelona
wamesonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya
kuwatandika Atletica bilbao usiku wa jana kwa mabao 3-1.
Barcelona waliwachapa Athletic Bilbao kwa mabao 3-1
kwa mabao ya Luis Suarez, Gerrard Pique na Neymer na hiyo barca kusonga mbele
kwa jumla ya mabao 5-2.
Nao Celta de vigo wakawaondoa katika michuano hiyo
vijana wa Diego Simione Atletico Madrid kwa kuwachapa kwa mabao 3-2.
Robo fainali ya pili itapigwa leo usiku kwa Las
Palmas kushuka dimbani kuwakabili Valencia, huku Mirandés wakiwa na kibarua
pevu dhidi ya Sevilla.
Post a Comment