kijana Said Khalid
Mlinda mlango chipukizi Said Khalid Kipao ambaye
yupo katika kituo cha kukuzia vipaji vya makipa kilichopo chini ya Mlinda
mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Peter Manyika
anatarajia kuondoka nchini February mosi mwaka huu kuelekea nchini Msumbiji
kwaajili ya kufanya majaribio katika klabu ya Quelimane inayoshiriki ligi kuu
ya nchini humo.
Akizungumzia safari yake hiyo kijana Saidi amesema
anamshukuru mwalimu wake Manyika ambaye ni msaada mkubwa wa safari yake hiyo
kwa kumuamini hadi kushawishika kumpeleka nchini Msumbiji na atajitahidi kufata
yale aliyoelekezwa alipokuwa kituoni hapo.
Naye Peter Manyika ambaye ni mwalimu wa kituo hicho
amesema kijana huyo amepata bahati ya kwenda katika klabu hiyo ambayo
inashiriki ligi kuu katika mji wa primeiro de Maio uliopo nchini Msumbiji na ni
mategemeo yake atafanya vizuri kulinga na kituo chake kutoa makipa chipukizi
wenye viwango vya juu zaidi.
Manyika amesema kabla ya Mwasongwe kwenda nchini
Msumbiji lakini pia kuna mlinda mlango mwingine chipukizi kutoka katika kituo
chake ambaye nae anaelekea nchini huo siku ya kesho kwaajili ya kufanya
majaribio katika klabu nyingine.
Post a Comment