Man City imekua timu ya pili kufuzu fainali ya
mchezo wa kombe la Capital baada ya kuichapa Everton kwa mabao 3-1.
Everton ndio walikua wa kwanza kuzifuma nyavu za Man
City baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu yake bao la kuongoza katika
dakika ya 18 ya mchezo.
Kiungo kutoka Brazil Fernandinho akasawazisha bao
hilo kwa shuti kali baada ya kutoka piga nikupige kwenye goli la everton katika
dakika ya 25.
Kevin De Bruyne akaongeza bao la pili baada ya kunganisha
krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na Raheem Sterling, kisha Sergio
Aguero kun, akahitimisha kazi kwa bao la tatu.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Goodson Park
Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1.
Man City watachuana na Liverpool katika mchezo wa
fainali utaofanyika Februari 28 katika dimba la Wembley.
Post a Comment