
Gwiji wa zamani wa klabu ya soka ya
Liverpool Jamie Carragher ameanza kuichambua Arsenal na kusema kuwa pasi nyingi
za mabao za kiungo Mesut Ozil zitakuwa si kitu iwapo Arsenal itashindwa
kunyanyua taji la Ligi ya Uingereza mwezi Mei mwaka huu.
Mjerumani huyo ametajwa kuwa
mchezaji wa Arsenal aliyefanya kazi kubwa msimu huu, baada ya kufikisha pasi 16
zilizozaa magoli, ni tishio sasa kwani anakaribia kuvunja rekodi ya Thierry
Henry ya pasi 20.
Hata hivyo, nahodha wa zamani wa
Liverpool, Carragher amesisitiza kuwa vijana hao wa Arsene Wenger wanahitaji
kushinda taji kubwa la Uingereza ili kuifanya kazi nzuri ya Ozil ionekane kuwa na
tija.
“Hesabu zake zinaonekana Anaelekea
kuvunja rekodi lakini kama hatapata medali, itakuwa na maana gani?",alisema
Carragher.
Washika Mtutu wamejitwalia Kombe la
FA mfululizo tangu ujio wa Ozil mnamo 2013, Lakini Arsena ina changamoto kubwa
ya kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza ambao waliutwaa kwa mara ya mwisho
2004.
Post a Comment