
Kiungo wa zamani wa klabu ya
Liverpool Steven Gerrard amesema mwaka huu ni mwaka wa mwisho kucheza soka sasa
atatundika daruga na kuuugeukia ukocha.
Gerrard amesema ifikapo November
2016 anampango wa kuachana na kazi yake ya kusukuma soka na kuanza kufundisha
mpira.
Gwiji huyo ambae alikuwa Nahodha
katika klabu yake ya Liverpool kabla hajajiunga na LA Galaxy ya nchini Marekani
ametwaa kombe la Champions League, Uefa Cup, FA Cup na League Cup.
“sina asilimia 100 lakini nafikiria
utakuwa ni mwaka wangu wa mwisho kusakata kabumbu”,Alisema Gerrard.
Kiungo huyo mwenye miaka 25 alikuwa
akijifunza kila siku jinsi ya kuiendesha timu na anauhakika kocha wa sasa wa
Liverpool Jurgen Klopp atamrudisha Anfield kujiunga naye.
Post a Comment