
Huu ni uwanja wa klabu ya soka
ya Yanga uliopo maeneo ya Jangwani wala sio bwawa kama unavyofikiria na klabu
hii hivi sasa ni klabu kongwe nchini tangu kuanzishwa mwaka 1935.
Sasa kutokana na mvua zinazoendeea kunyesha katika sehemu
tofauti tofati za nchi KILOWOKO.BLOGSPOT.COM imeshuhudia uwanja huo wa mabingwa hao wa ligi
kuu soka Tanzania bara kwa mwaka 2014-15 klabu ya Yanga ukiwa katika hali mbaya
baada ya maji kujaa katika uwanja huo.
Uwanja wa mabingwa hao umekuwa ni sehemu ya
kuhifadhi maji baada ya uongozi wa klabu hiyo kushindwa kutengeneza miundombinu
bora inayoweza kupitisha maji hayo.
Hali hii imekuwa ikijitokeza kila mwaka hivi sasa
huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa hauna mipango ya kuurekebisha uwanja huo ambao
hutumika na wachezaji wa klabu yao kwaajili ya kufanyia mazoezi, hali
inayosababisha wakati mwingine wachezaji hao kuukwepa uwanja huo kutokana na
maji kujaa.
Post a Comment