
Ligi Daraja la Kwanza kwa siku ya kesho kwa michezo
12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku timu 3 za juu kutoka katika kila
kundi zikipata nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao moja moja.
Kundi A, Jumamosi Mji Mkuu watawakabili Africa Lyon
uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, KMC dhidi ya Kiluvya uwanja wa Mabatini
Mlandizi, Polisi Dodoma watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Mgambo Mpwapwa, huku Jumapili Polisi Dar
wakiwakaribisha Ashanti uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi B, Njombe Mji watakua wenyeji wa Kimondo
uwanja wa Amani Njombe, Lipuli FC dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi – Mafinga,
Uwanja wa Majimaji mjini Songea JKT Mlale watakua
wenyeji wa Polisi Morogoro, huku Jumapili kukichezwa mchezo mmoja Ruvu Shooting
dhidi ya Burkinafaso uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Kundi C, Rhino Rangers watawakaribisha JKT Kanembwa
uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Panone FC dhidi ya Geita Gold uwanja wa
Ushirika mjini Moshi, uwanja wa Karume Musoma, wenyeji Polisi Mara watacheza
dhidi ya Polisi Tabora, huku siku ya Jumapili Mbao FC wakiwakaribisha JKT
Oljoro uwanja wa CCM Kirumba.
Post a Comment