
Klabu ya soka ya Liverpool ipo katika mazungumzo ya
kutwaa kiungo wa klabu ya soka ya Shakhtar Donetsk's raia wa nchini
Brazili Alex Teixeira katika kipindi hiki cha usajili barani ulaya.
Klabu ya Liverpoool ipo tayari kulipa kiasi cha £24.5m
kwa ajili ya kutwaa mchezaji huyo mwenye miaka 26 katika viunga vya Anfield.
Hata hivyo Liverpool watakuwa na kibarua kizito
baada ya mchezaji Teixeira huyo pia kutakiwa na klabu ya Chelsea kwa ada ya
uamisho wa £39m.
Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anaangaika
kutafuta kiungo mshambuliaji hivi sasa baada ya wachezaji wake Danny Ings, Divock
Origi Daniel Sturridge kuwa majeruhi.
Baada ya kumsajili Christian Benteke kwa £32.5m Liverpool
wamefunga mabao 25 pekee kipindi katika michezo 22 ya ligi kuu soka nchini
Uingereza katika kipindi hiki.
Teixeira hadi hivi sasa tayari ameshapachika mabao 22
katika michezo 15 ya ligi na mabao 4 katika michezo 10 ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya msimu huu.
Post a Comment