
Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha
kuwa kuwa nyota wake waliokuwa majeruhi Alexis sanchez na Mesut ozil wako tayari
kuwavaa Chelsea siku ya Jumapili.
AWenger amesema kuwa Sanchez na Ozil watakuwepo
katika mchezo huo muhimu ambao unasubiri sana na mashabiki wa soka dunia kote..
Vinara hao wa Ligi Kuu walicheza bila ya Sanchez
ambaye amefunga mabao sita msimu huu, toka Novemba mwaka jana baada ya kupata
majeruhi ya msuli wa paja.
Huku Ozil yeye alikosa mchezo wa ligi uliopita dhidi
ya Stoke City uliomalizka kwa sare ya bila kufungana, baada ya kusumbuliwa na
majeruhi ya kidole gumba.
Wenger aliendelea kudai kuwa kiungo Francis Coquelin
amerejea katika mazoezi kamili toka aumie katika mchezo dhidi ya West Bromwich
Albion Novemba mwaka jana wakati Danny Welbeck ambaye hajacheza msimu huu naye
akitarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo.
Post a Comment